Matthew 22:34-39

34 aMafarisayo waliposikia kwamba Isa alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja. 35 bMmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema, 36“Mwalimu, ni amri ipi katika Torati iliyo kuu kuliko zote?”

37 cIsa akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 dNayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’
Copyright information for SwhKC